E-bok, Engelska, 2026
OKTOBA 29 NA VITA VYA ALGORITHM Ujasusi wa Kisasa: Teknolojia, Propaganda na Rasilimali Dhidi ya Uhuru wa Mataifa
Av Sado Faraji
67 kr
Läs direkt i Bokus Reader – eller ladda ned till din enhet
Beskrivning
Ni nini hasa kilitokea Tanzania tarehe 29 Oktoba 2025?OKTOBA 29 NA VITA VYA ALGORITHM ni uchambuzi wa kina wa namna teknolojia, mitandao ya kijamii, propaganda, upotoshaji wa habari na siasa za kimataifa zinavyoweza kubadilisha mazingira ya kisiasa na kiusalama ya taifa.Kupitia matukio ya kuelekea na baada ya Oktoba 29, 2025, Sado Faraji anachunguza uwanja mpya wa mapambano ambao haupo kwenye barabara pekee, bali pia kwenye simu, mitandao, akili za wananchi na mifumo ya taarifa.Kitabu kinachunguza vita vya mseto, misinformation, disinformation, AI na deepfakes, udukuzi wa taarifa, ushawishi wa mitandao ya kijamii na namna maudhui ya kidijitali yanavyoweza kutengeneza taharuki na kubadili mitazamo ya jamii.Lakini uchambuzi hauishii hapo. Kitabu kinaunganisha matukio ya Tanzania na historia ya Operation Ajax nchini Iran, ushindani wa kimkakati kati ya Marekani na China, na umuhimu unaoongezeka wa rare earth minerals na rasilimali nyingine muhimu za Tanzania katika siasa za usalama wa dunia.Je, matukio ya Oktoba 29 yalikuwa mlipuko wa kawaida wa kisiasa? Au yalikuwa sehemu ya mazingira mapana zaidi ambamo vita vya taarifa vilikutana na matukio ya ardhini?Kitabu hiki hakitoi majibu mepesi. Kinachunguza ushahidi, kinaweka historia katika muktadha, na kinauliza maswali ambayo Tanzania haiwezi kuyapuuza katika enzi ya algorithms, AI na vita vya akili.Oktoba 29 haikuwa tu siku ya uchaguzi. Inaweza kuwa somo la aina mpya ya vita.
Produktinformation
- Utgivningsdatum: 2026-04-29
- Språk: Engelska
- Filformat: EPUB
- Kopieringsskydd: LCP
- ISBN: 9798235224629
- Förlag: Distributed via Draft2Digital
Utforska kategorier
- Inga kategorier tillgängliga.
Betyg & recensioner
0 recensioner
Inga recensioner tillgängliga.